
Baadhi ya wanafunzi na Walimu wa Shule ya Bwawani walitembelea Gereza la Mifugo Ubena, lililopo Bwawani kutoa misaada ya kijamii kwa Wafungwa Gerezani hapo na kujifunza namna ambavyo Wafungwa wanalelewa na kufunzwa tabia njema kwa lengo la kuwafundisha Wanafunzi kuwa na Wananchi wema (Good citizens) na kuwahamasisha kujenga tabia ya kuwasaidia watu wahitaji katika jamii.